ZINAZOVUMA:

Hatua dhidi ya Niger ni maamuzi ya ECOWAS

Raisi wa Nigeria Bola Tinubu amesema kuingilia kijeshi nchini Niger...

Share na:

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amejibu shutuma zilizokua zikimkabili kuhusu uamuzi wa kuingia Niger kijeshi na kusisitiza kuwa uamuzi wa kuingilia kijeshi ni hatua ya mwisho iliyotolewa na viongozi wa ECOWAS na sio mamlaka ya Nigeria.

Haya yanajiri wakati kiongozi huyo wa Nigeria ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS akishutumiwa kwa madai ya kuingilia kijeshi nchini Niger.

Katika taarifa, msemaji wa serikali ya Nigeria alisisitiza kuwa Rais ameona ni muhimu kusema kwamba mamlaka na maamuzi yaliyotolewa na ECOWAS ni msimamo wa ECOWAS na sio Nigeria.

Taarifa hiyo pia inasema vikwazo vya kifedha vilivyowekewa Niger pia ni vya ECOWAS na sio serikali ya Nigeria.

ECOWAS imesema inapendelea azimio la kidiplomasia na kisiasa lenye lengo la kumrejesha madarakani Rais aliyechaguliwa nchini Niger Mohamed Bazoum ambaye aliondolewa madarakani kwa mapinduzi lakini ikasema uingiliaji kati wa kijeshi utakuwa chaguo la mwisho, iwapo serikali ya kijeshi itaendelea kukaidi.

Kufuatia kumalizika kwa muda wa uliotolewa na ECOWAS kwa Niger, Viongozi wa nchi hizo za Magharibi wanatarajia kukutana tena Alhamisi huko Abuja nchini Nigeria ambapo mazungumzo kuhusu hatua inayofuata nchini Niger yatafanyika.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya