Jimbo la kaskazini mwa India la Himachal Pradesh limekuwa likishuhudia mvua kubwa katika siku chache zilizopita na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika eneo la milima.
Maji yanayotiririka yanaharibu madaraja, kusomba nyumba na magari, na kusababisha uharibifu mkubwa katika jimbo hilo.
Jimbo jirani la Uttarakhand liko katika hali sawa na viwango vya maji vya mito kadhaa katika eneo hilo ambalo vimevuka alama ya hatari.
Zaidi ya watu kumi na mbili wamekufa katika siku tatu zilizopita kaskazini mwa India kutokana na mafuriko hayo.