ZINAZOVUMA:

GEREZA LA KOBONDO LABUNI MKAA KWA MARANDA

Share na:

Jeshi la Magereza wilayani Kibondo, mkoani Kigoma, limeanza kutumia mkaa mbadala unaotokana na mchanganyiko wa maranda ya miti na udongo. Mkaa huo unaozalishwa ndani ya Gereza la Kibondo, kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali la matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mafanikio hayo yamebainika wakati wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, walipotembelea gereza hilo kwa lengo la kukagua na kujionea utekelezaji mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika taasisi za umma nchini.

Mkuu wa Gereza la Kibondo, Bw. Peter Shabani, amesema gereza hilo lilichukulia agizo la Serikali kama fursa ya ubunifu na kujitegemea kwa kutumia rasilimali zilizopo hatua ambayo inalenga kulinda afya, mazingira na kupunguza gharama za matumizi ya nishati.

Endelea Kusoma