Muungano wa chama tawala cha kisiasa kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umemteua Rais Felix Antoine Tshisekedi kuwa mgombea wao wa urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 20 Disemba.
Baada ya kushinda uchaguzi uliokuwa na utata wa mwaka 2018, Tshisekedi sasa anapigania muhula wake wa pili katika taifa hilo ambalo ni mzalishaji mkubwa wa madini ya Cobalt na Shaba.
Utawala wake umekumbwa na changamoto kuu za kiuchumi, janga la UVIKO-19, mripuko wa ugonjwa wa Ebola na ukosefu wa usalama, hasa upande wa Mashariki kulikoibuka tena kwa kundi la wanamgambo la M23.
Kundi hilo limefanikiwa kuchukua mamlaka katika maeneo kadhaa na kusababisha kuyumba kwa mahusiano ya Congo na jirani yake Rwanda inayodaiwa kuliunga mkono kundi hilo.