ZINAZOVUMA:

Elon Musk amempata Boss mpya wa Twitter

Bilionea Elon Musk amesema kwamba amempata Mtendaji Mkuu mpya atakae...

Share na:

Bilionea na mmiliki wa twitter Elon Musk amesema kwamba amempata Mtendaji Mkuu mpya wa kuongoza mtandao huo.

Elon Musk ametangaza habari hizo kwenye mtandao wa kijamii, alioununua mwaka jana kwa Dola za kimarekani bilioni 44.

Hata hivyo Musk hakumtaja Mkuu mpya wa mtandao huo lakini amesema angeanza baada ya wiki sita, ambapo atakuwa Mwenyekiti Mtendaji na Afisa Mkuu wa teknolojia.

Ikumbukwe Elon Musk amekuwa chini ya shinikizo la kutaja mtu mwingine kuongoza kampuni na kuzingatia biashara zake nyingine.

Hii ilitokea mwaka jana baada ya watumiaji wa Twitter kumpigia kura ya kumtaka aachie ngazi katika kura ya maoni mtandaoni, japo alijibu kuwa “Hakuna anayetaka kazi hiyo ambaye anaweza kuiweka Twitter hai.”

Hata hivyo baadae mnamo Februari alitangaza anaweza kuteua Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Twitter kufikia mwisho wa 2023.

Musk pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kutengeneza magari ya umeme ya Tesla na mtengenezaji wa vyombo vya angani, na kampuni ya mawasiliano ya satelaiti ya SpaceX.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya