Bunge la Knesset nchini Israel limepiga kura na kupitisha muswada wa kupunguza mamlaka juu ya mahakama kuu na kulifanya Bunge kuwa na maamuzi ya mwisho.
Uamuzi huo wa Bunge la Knesset, utabadilisha mfumo mzima kiutendaji wa Mahakama Nchini humo pamoja na kupunguza Mamlaka yake.
Licha ya maandamano makubwa kutoka kwa upinzani wanaopinga mabadiliko hayo lakini uamuzi huo hatimae ulifikiwa.
Mapendekezo yaliyopo kwenye Muswada wa Sheria hiyo yataruhusu Bunge kubatilisha uamuzi wowote wa Mahakama Kuu hasa kwenye masuala yanayohusu Serikali, pia Bunge litakuwa na uamuzi wa mwisho katika kuchagua Majaji.