ZINAZOVUMA:

Biden asitisha uwekezaji wa teknolojia China

Raisi wa Marekani Joe Biden ametia saini agizo linalozuia makampuni...

Share na:

Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa Rais wake Joe Biden ametia saini agizo linalozuia uwekezaji wa teknolojia nchini China na nchi nyingine.

Agizo la kuzuia uwekezaji katika teknolojia linasema kuwa makampuni ya Marekani hayataweza tena kuwekeza nje ya nchi katika mifumo ya juu zaidi, kama vile akili bandia (AI) au kompyuta katika nchi zenye matatizo hasa ikitajwa China.

Uamuzi huo uliochukuliwa kwa jina la ulinzi wa usalama wa taifa wa Marekani, unaonyesha hofu ya wazi ya utawala wa Biden ukihofia China itanufaika na uwekezaji wa Marekani katika suala la uhamisho wa teknolojia, kubadilishana maarifa na upatikanaji wa masoko.

Aidha Kwa upande wa China haijafurahishwa sana na inapinga vikali msisitizo wa Marekani wa kuweka vikwazo kwa uwekezaji nchini humo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya