Mkutano wa awali wa Baraza jipya la NATO na Ukraine unaotarajiwa kushughulikia usalama wa Black Sea umepangwa kufanyika Jumatano.
Taarifa hii imetolewa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika hotuba yake Jumapili usiku.
Msemaji wa NATO Oana Lungescu alisema kwamba mkutano huo ulioombwa na Zelenskyy utajadili hali hiyo kufuatia kujiondoa kwa Urusi katika mkataba wa mwaka mmoja wa kusimamia mauzo ya nafaka kutoka bandari za Ukraine.
Aliongeza kusema kwamba mkutano huo ni miongoni mwa matukio ambayo Ukraine inajiandaa kwa ajili ya wiki ijayo ambao utaimarisha ulinzi wa nchi hiyo.
Aidha aliweka wazi kuwa misaada mipya inatayarishwa ikiwa ni pamoja na ulinzi zaidi wa anga mizinga na silaha za masafa marefu