Mchezaji wa AC Milan na Raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ametangaza kustaafu kucheza soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 41.
Ibrahimovic alitangaza hatua yake hiyo baada ya mchezo wa mwisho wa kumaliza msimu huu mbele ya umati wa mashabiki.
Katika maisha yake ya soka Zlatan Ibrahimovic alifunga jumla mabao 511 katika vilabu mbalimbali alivyowahi kuvichezea ikiwemo PSG, Manchester United, Ac Milan na Inter Milan.
Ibrahimovic alifanikiwa kushinda jumla ya mataji 34 katika taaluma yake hiyo ya soka na alibahatika kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Ballon d’Or mara 11.