Klabu ya Yanga imezindua jezi mpya za msimu wa 2023/2024 nchini Malawi na kumkabidhi Rais Samia Suluhu Hassani pamoja na mwenyeji wake Rais wa Malawi, Lazarus Mccarthy Chakwera.
Klabu hiyo iko nchini humo kwa mwaliko wa Rais Chakwera kwa ajili ya kutoa burudani ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimiaho ya miaka 59 ya uhuru wa nchi hiyo.
Mchezo huo utachezwa leo tarehe 6, 2023 dhidi ya klabu ya Nyasa Big Bullets ya nchini humo.
Aidha klabu mbalimbali nchini zimeweka wazi kuwa tayari jezi za msimu mpya zimekamilika na wanasubiri wakati sahihi tu wa kuzindua jezi hizo.
wakati hayo yakiendelea pia utambulisho wa wachezaji wapya umeendelea ambapo mpaka sasa Azam wametambulisha wachezaji wapya wanne, Simba mchezaji mmoja huku wakiahidi kuendelea Leo hii ifikapo saa saba mchana na Yanga pia wakitambulisha mchezaji mmoja mpaka sasa.