Majira ya saa tano Asubuhi Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima
ameitambulisha klabu ya Yanga kama mabalozi wa kupambana na mmomonyoko wa maadili sambamba na unyanyasaji wa kijinsia
“Napenda kuchukua fursa hii kuwatambulisha rasmi Klabu ya Young Africans SC kuwa Mabalozi wa kampeni ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto” Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima
Hata hivyo Rais wa Yanga Sc, Injinia Hersi Said aliongezea kuwa
“Naungana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika kampeni ya kupinga mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto”.
Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said