Shirika la Afya Duniani (WHO), limeridhia kuanza matumizi i ya chanjo ya pili ya ugonjwa wa malaria kwa watoto, ambayo inaweza kuokoa maisha ya maelfu endapo kutakuwa na uwezekano wa kuziba pengo kubwa la usambazaji na mahitaji.
DW Swahili imeripoti kuwa, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amenukuliwa akisema “Kama mtafiti wa malaria, nilikuwa na ndoto ya siku ambayo tutakuwa na chanjo salama na yenye ufanisi dhidi ya malaria. Sasa tuna mbili.”
Imeelezwa kuwa chanjo hiyo mpya ya R21/Matrix-M, iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza na kuzalishwa na taasisi ya Serum ya India, tayari imeidhinishwa kutumika katika nchi tatu za Afrika ambazo ni Burkina
Faso, Ghana na Nigeria.