Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji, amewataka maofisa biashara wote nchini kukagua bei ya sukari duka kwa duka na atakayepatikana akiuza kilo moja kwa zaidi ya Sh 3,200 achukuliwe hatua za kisheria.
Waziri Kijaji ameyasema hayo alipotembelea kiwanda cha kuzalisha cukari cha TPC mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto walizonazo.
Dkt Kijaji amesema ni jukumu la maofisa biiashara kutambua mfanyabiashara yeyote atakayeuza sukari juu ya bei kati ya Sh 2800 na Sh 3200 kumchukulia hatua.
Amesisitiza kuwa ni jukumu la serikali kulinda bidhaa yoyote inayotengenezwa nchini na kufanya juhudi za kila namna, ili kuwasaidia wawekezaji na wafanyabiashara kuwa na mazingira bora na wezeshi, ili kukuza biashara zao na kuwa na tija.