ZINAZOVUMA:

Wanajeshi wa Afrika Kusini walalamikia ukosefu wa vifaa DRC

Wanajeshi wa Afrika Kuisni waliopelekwa nchini DRC kwa ajili ya...

Share na:

Wanajeshi wa Afrika Kusini waliopelekwa DRC kusaidia kuleta utulivu wanasema baadhi yao hawana silaha, na wanatarajiwa kupambana na waasi wa M23 bila msaada wa helikopta za usafiri.

Mwezi Februari, serikali ya Afrika Kusini ilipeleka wanajeshi 3,000 kujiunga na wengine 1,000 ambao tayari walikuwa katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linalokumbwa na vita.

Wakati huo, Pretoria ilisema kupelekwa kwa wanajeshi hao ilikuwa sehemu ya dhamira yake ya kulinda amani barani Afrika, na kuisadia DRC kukabiliana na mashambulizi ya waasi.

Lakini sasa, wanajeshi hao wanasema hawana vifaa vya msingi, na kuwaweka katika hatari kubwa.

Afrika Kusini inakabiliwa na changamoto kadhaa za kiuchumi.

Waziri wa ulinzi, Thandi Modise, aliwambia waandishi wa habari hivi karibuni mjini Pretoria kwamba helikopta tano tu za usafiri kati ya 39 ndizo zinafanya kazi, na kwamba ni helikopta tatu tu kati ya 11 za kufanya mashambulizi ndizo zinaweza kuruka.

Wizara yake inakiri kuwa ilishindwa kusaini kandarasi mpya na kampuni ya kutunza na kukarabati ndege hizo.

Wanajeshi nchini DRC wanasema pia kwamba hawapati huduma za madaktari na waaguzi, na wakati mwingine hulala njaa baada ya kukosa chakula.

Kiongozi wa chama cha jeshi la taifa Pikkie Greeff, anasema serikali ilipeleka wanajeshi wake katika moja ya maeneo hatari zaidi ya vita duniani bila vifaa, ufadhili na mafunzo muhimu.

“Wanajeshi wa Afrika Kusini wanalazimika kuweka kambi mpya, wakiwa pia na fikra ya kushambulia sio kujilinda. Hiyo ni njia mpya ya kujifunza kwa jeshi kwa sababu hatujafanya mazoezi hayo. Usipofanya mazoezi mara kwa mara, hautatekeleza vizuri. Kando na hayo, kuna changamoto za kifedha mbali na uwezo wa wanajeshi hawa. Hakuna ndege ya kubeba vifaa muhimu ambavyo wanajeshi wanahitaji walipopelekwa ili kuwasaidia kikamilifu,” alisema.

Tangu mwezi Februari, waasi wa M23 wameua wanajeshi kadhaa wa Afrika Kusini wanaopigania ardhini, na kujeruhi wengine kadhaa katika shambulio la kombora.

Greeff anasema anazungumza na wanajeshi walioko DRC kila siku, na ari yao iko chini. Anasema wengine wanahisi kwamba wako katika “operesheni ya kujiua.”

“Watu hawa wako katika hatari kubwa. Kupelekwa kwao kuliamualiwa kwa haraka sana. Kama kulikuwa mpango, mpango huo haukujadiliwa kwa uwazi kwa sababu kwa hakika wanajeshi walio uwanjani wanaachwa katika hali ngumu kwa sababu ya uhaba huu wa vifaa na mambo mengine. Hali ni tete sana,” aliongeza.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya