ZINAZOVUMA:

Waliyosema serikali kuhusu uraia pacha

Suala la uraia Pacha bado halijafikiwa muafaka nchini Tanzania, wapo...

Share na:

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Stergomena Tax amesema suala la uraia pacha halina mwafaka wa pamoja kitaifa na kimataifa.

Dkt Tax alisema hayo bungeni Dodoma wakati anahitimisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2023/24.

“Bado suala hili la uraia pacha halina mwafaka wa pamoja, sio nchini kwetu tu lakini hata nchi za nje, lakini kwa kutambua umuhimu wa diaspora walioko nje Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha wanapata haki,” alisema.

Dk Tax alisema takwimu zinaonesha nchi 49 tu ambazo zinakubali na kutoa uraia pacha na kusisitiza kuwa endapo Tanzania itatoa basi wananchi wake walio nje ya nchi wanaweza kukosa baadhi ya fursa.

“Endapo Tanzania tukitoa uraia pacha kwa sasa hivi wakati hakujawa na mwafaka kitaifa na kidunia kuna wale wanaoweza kukosa fursa kwenye nchi ambazo Diaspora zipo na zile nchi hazitambui uraia pacha,” alisema.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya