ZINAZOVUMA:

Waliopanga maandamano waonywa

Mkuu wa Jeshi la polisi IGP Camillius Wambura amewaonya wale...

Share na:

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura amewaonya watu wanaopanga kuandamana ili kuiangusha Serikali akisema wasijaribu kutingisha kiberiti kwa kuwa polisi wapo imara kukabiliana nao.

Wambura ametoa onyo hilo, baada ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii inayohusu kundi la watu wenye nia kuandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha Serikali kabla ya mwaka 2025.

Wambura ametoa onyo hilo, leo Ijumaa Agosti 11, 2023, wakati akizungumza na wanahabari, ambapo amesema kundi hilo linahusisha maandamano hayo na kushawishi Watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za bandari.

“Tuliamini hoja za bandari zinajibiwa kwa hoja, tukaamini baadhi ya watu walikwenda mahakamani basi wangeheshimu uamuzi wa mhimili huo, lakini badala yake wametoka na kutafuta ushawishi wa kuwachochea Watanzania kuwaunga mkono,” amesema na kuongeza;

“Mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanaiangusha Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya mwaka 2025. Nimewaita hapa kuwaambia wakome kabisa na kusitisha matamshi yao ya kichochezi na tutawachukulia hatua za kisheria,” amesema Wambura.

Jana Agosti 10, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imetoa uamuzi mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA), ikisema hauna tatizo hivyo pingamizi lililowekwa na walalamikaji halina mashiko.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya