ZINAZOVUMA:

Waliofutiwa matokeo kidato cha nne kurudia mtihani.

Wizara ya elimu imetoa nafasi kwa wanafunzi 337 waliofutiwa matokeo...

Share na:

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa maelekezo kwa wanafunzi 337 ambao matokeo ya kidato cha nne mwaka 2022 yalifutwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Kuomba kurudia tena kufanya mtihani. Matokeo ya wanafunzi hao yalifutwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jana Aprili 11,2023 Jijini Dodoma Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda, amesema kati ya wanafunzi 337,wanafunzi 333 walifutiwa matokeo kutokana na udanganyifu huku wanafunzi 4 wakifutiwa matokeo kutokana na kuandika matusi katika mitihani yao.

Prof.Mkenda amebainisha kuwa utaratibu wa kurudia mitihani hiyo kwa wanafunzi hao utakwenda sambamba na mitihani ya kidato cha sita ambao unatarajiwa kuanza Mei 2,2023, hivyo watawekewa utaratibu wa kuchanganyika pamoja wakati wa kurudia mitihani hiyo.

Pia amewataka watanzania kwa kukemea kwa pamoja matukio ya wizi wa mitihani kwani inafundisha watoto udanganyifu na wizi, inaondoa uweledi na kuwanyima haki watahiniwa ambao hawajashiriki katika wizi huo ila wamefaulu kwa jitihada zao wenyewe.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya