Mamlaka za nchini Kenya siku ya Jumapili ilisema watu tisa zaidi walipoteza maisha yao katika saa 24 zilizopita, kutokana na mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa.
Ongezeko la vifo vya watu tisa limefanya idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko hayo 228.
Taarifa hiyo ya Wizara ilifafanua kuwa kimbunga Hidaya kilipoteza nguvu, baada ya kutua katika Kisiwa cha Mafia nchini Tanzania siku ya Jumamosi.
Wizara hiyo ilisema kuwa, kutokana na Kimbunga Hidaya shughuli za ufukweni kama uvuvi, kuogelea na usafiri uiso wa lazima zimepigwa marufuku hadi tarehe Mei 6.
Pia wizara hiyo imebainisha kuwa dhoruba ya Kimbunga Hidaya imekamilika na kinatabiriwa kupungua kidogo kidogo.
Ila mvua zitaendelea kunyesha katika maeneo ya pwani, huku upepo mkali na mawimbi makubwa yameshuhudiwa maeneo ya Kaunti ya Kwale.
Mvua hizi pia zimeathiri zaidi ya watu takriban 227,238 na shule karibu 1,967 zikiathiriwa na mafuriko.