ZINAZOVUMA:

Wakenya wahamaki muda wa Rais madarakani kuongezwa

Hisia kali zimeibuka nchini Kenya baada ya Seneta mmoja kupendekeza...

Share na:

Seneta nchini Kenya ambaye ni mwanachama wa muungano unaotawala amependekeza kuongezwa kwa muda wa ukomo wa muhula wa Urais kutoka miaka mitano hadi saba.

Kauli yake hiyo imezua hisia kali nchini humo na kuonekana kama ni njama ya serikali kutaka kuongeza muda wa Rais kukaa madarakani.

Seneta wa Nandi Samson Cherargei amesema Rais William Ruto, ambaye amekuwa afisini kwa takriban mwaka mmoja, huenda akakosa muda wa kutosha kutekeleza ilani yake ya kampeni.

Hata hivyo, pendekezo hilo limezua hisia kali miongoni mwa baadhi ya Wakenya huku upinzani ukishutumu serikali kwa kupanga njama ya kuondoa ukomo wa mihula ya urais.

“Badala ya kuongeza inafaa ipunguzwe hadi miaka minne kila muhula .Hii ndiyo njia pekee ya uhakika ya kuleta uwiano wa kitaifa na kuzuia maslahi binafsi hivyo kuruhusu utii wa katiba kutekelezwa kikamilifu,” aliandika mmoja wa raia wa Kenya kwenye mtandao wa X.

“Iwapo kiongozi yeyote hawezi kutekeleza ilani yake katika kipindi cha miaka 10, kuna haja gani ya kuongeza minne zaidi?”raia mwingine aliandika.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya