Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane Zulu amesema unywaji Pombe husababisha Madhara kwenye ubongo wa watoto na hivyo wanaokunywa wakati wa ujauzito washtakiwe kwa unyanyasaji wa watoto.
Akizungumza katika kongamano la kukuza uelewa kuhusu athari za pombe kwa watoto, amesema Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitaja Afrika Kusini kuwa na kiwango cha juu zaidi cha walevi duniani.
Kwa mujibu wa takwimu, matumizi ya pombe nchini humo yameripotiwa kufikia 41.5% kwa wanaume na 17.1% kwa wanawake. Wakazi wa Mijini ni 33.4% na wa vijijini 18.3%).