ZINAZOVUMA:

Wafanyabiashara wa mahindi waliokwama Zambia waachiwa

Shehena za mahindi zilizokuwa zimekwama mpakani mwa Tanzania na Zambia...

Share na:

Hatimaye shehena ya mahindi iliyokuwa imekwama nchini Zambia, yaruhusiwa kuingizwa nchini baada ya Serikali ya Tanzania na Zambia kutatua changamoto hiyo kidipromasia ili kuimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt Francis Michael alipotembelea mpaka wa Tunduma na kuzungumza na wafanyabiashara wa Kitanzania ambao waliweka kambi mpakani hapo wakiendelea na jitihada mbalimbali za kukomboa shehena hiyo.

Dkt Michael amesema kuwa zaidi ya malori 30 ambayo ni sawa na Tani 1000 za mahindi yalikwama katika mji wa Nakonde Zambia, lakini sasa yameruhusiwa kuvuka ikiwa ni hatua za awali za kuruhusu mahindi yote yaliyokwama nchini humo kuruhusiwa.

Inadaiwa kuwa mahindi hayo yalinunuliwa na wafanyabiashara hao kwa kusudi la kuyaingiza nchini miezi sita iliyopita, kwa kuzingatia taratibu zote za nchi hiyo, lakini baadaye kutokana na nchi hiyo kuona inakabiliwa na upungufu wa chakula mwaka huu, ilifunga mpaka na hivyo kuzuia mazao ya nafaka kutoka nje.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya