Wadau wa mfuko wa Afya wamechangia kiasi cha shilingi Bilioni 37.7 kupitia ufadhili wa Moja kwa moja wa kituo cha afya (DHFF), (2021-2025) ili kusaidia kutokomeza malaria nchini ifikapo mwaka 2030.
Hayo yamesemwa na waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu jijini Dodoma wakati akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot ambao ni Moja ya wadau hao.
Waziri Ummy amemshukuru balozi huyo kwa msaada huo na ahadi ambazo zimetolewa na Uswisi katika kusaidia sekta ya afya kupitia michango mbalimbali ya ruzuku
Amesema lengo la mradi ni kuchangia kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030 kupitia ushirikishwaji wa wadau wa kitaifa, kisekta na kikanda kwa kushawishi mijadala ya sera za kimataifa na miongozo ya kiufundi.
Aidha waziri Ummy ameiomba serikali ya Uswisi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutokomeza magonjwa ya ngono na VVU.
Pamoja na mimba zisizotarajiwa, ukatili wa kijinsia pamoja na kusaidia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii (CHWs).
Kwa upande wake balozi wa Uswisi nchini Tanzania Didier Chassot amesema serikali ya Uswisi itaendelea kusaidia sekta ya afya nchini ili kudumisha umoja uliopo.