Vyombo vya habari vya eneo la Amhara nchini Ethiopia vimeripoti kuwa ndege ya jeshi la Ethiopia imewashambulia kwa mabomu waandamanaji katika mji huo na kuwauwa takribani ya watu 70.
Mashambulizi ya anga yanaripotiwa kuwakumba waandamanaji, ambao walikuwa wamekusanyika katika mji wa Finote Selam kupinga mipango ya vikosi vya serikali kuingia eneo hilo.
Hata hivyo mpaka sasa hakuna uthibitisha wa madai hayo na bado hakuna maoni yoyote kutoka kwa serikali mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Jeshi na kundi la wanamgambo, linaloitwa Fano wamekuwa wakihusika katika mapigano makali katika eneo la Amhara katika wiki za hivi karibuni.
Wanamgambo hao walikuwa wamekataa kujisalimisha na kusalimisha silaha, na kusababisha serikali ya shirikisho kupeleka jeshi.