Mteule wa Rais Wiliam Ruto wa Kenya, kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki Bi. Veronica Nduva anatatarajia kuapishwa siku ya ijumaa.
Bi. Nduva amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Jinsia na Hatua sawazishi nchini ya Kenya.
Pia Rais Ruto alimteua Jaji Zablon Muruka Mokua kuwa mmoja wa majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki, na ataapishwa kwa ajili ya kitengo cha kusikiliza Kesi mara ya Kwanza katika mahakama hiyo.
Jaji huyo alikuwa mjumbe wa Baraza la Kaunti ya Kisii, ameteuliwa kama mbadala wa Charles Nyachae ambaye amestaafu mwaka huu.
Katika teuzi hizo za Rais Ruto, uteuzi wa Zablon Mokua umepingwa na taasisi Jumuiya ya Wanasheria wa Kenya na ile ya Afrika Mashariki wakisema Wakili huyo hana vigezo vya kuwa katika nafasi hiyo.
Hata hivyo Waziri wa Afrika Mashariki nchini Kenya, alipoulizwa alisema kuwa jina la Wakili Mukoa halikuwako katika majina yaliyoletwa toka Kamisheni ya Mahakama.
Na kuongeza kuwa mamlaka ya kuteua mtu katika nafasi hizo amepewa Mkuu wa Nchi husika, na majibu haya yanaashiria kuwa huenda Wakili Mokua amependekezwa na Rais Ruto kushika nafasi hiyo.