Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa siku ya leo Alhamisi litafanya kikao cha dharura mjini Geneva kujadili mzozo unaoendelea nchini Sudan.
Kuna ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya raia, unyanyasaji wa kijinsia na uporaji wa hospitali.
Maelfu ya watu wamekimbia makazi yao na mashirika ya misaada yanasema hayawezi kufanya kazi kwa usalama nchini humo kufuatia mapigano yanayoendelea.
Mataifa kadhaa ya Afrika, ikiwemo Sudan, yanaripotiwa kusitasita kuhusu mkutano huo unaofanyika, wakihofia kuwa unaweza kuhatarisha mazungumzo yanayoendelea ya kusitisha mapigano.