Umoja wa Ulaya umewasilisha mpango wa dharura wa kuisaidia Italia kuweza kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi ambao mnamo wiki iliyopita walivunja rekodi baada ya kuwasili kwa wingi katika kisiwa chake cha Lampedusa.
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen jana Jumapili alikitembelea kisiwa cha Lampedusa ambacho kinapambana na ongezeko kubwa la wahamiaji wanaowasili na kuahidi mpango wa Umoja wa Ulaya wa kuisaidia Italia kushughulikia hali hiyo.
Mpango huo unajumuisha kutumia shirika la ulinzi wa mipaka la Umoja wa Ulaya Frontex kubaini wahamiaji wanaowasili Italia na kuwarejesha wale wasiokidhi vigezo.
Takribani wahamiaji 126,000 wamewasili Italia tangu mwaka huu unaze, ikiwa ni karibu mara mbili ya idadi kama hiyo kwa takwimu za mwaka jana.