ZINAZOVUMA:

Ugonjwa mpya (Marburg) waibuka bukoba.

Ugonjwa wa Marburg unasababishwa na virusi vya Marburg umegundulika huko...

Share na:

Wizara ya Afya nchini Tanzania kupitia waziri wake Ummy Mwalimu imethibitisha kuwepo kwa ugonjwa mpya wa “Marburg” ambao unasababishwa na virusi vya Marburg.

Waziri Ummy amesema maabara ya Taifa imethibitisha kuwepo kwa “MVD” Marburg virus disease ambao umesababisha vifo vya watu watano hadi sasa katika mkoa wa kagera.

Aidha ameainisha kuwa ugonjwa huu hauna tiba rasmi bali mgonjwa hutibiwa kulingana na dalili anazokuwa nazo, Dalili hizo ni pamoja na homa, kutokwa na damu, kutapika pamoja na figo kushindwa kufanya kazi.

Mpaka sasa ni wagonjwa nane ambao wamethibika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huu wa Marburg na kati ya hao watano wamepoteza maisha na watatu wanaendelea na matibabu.

Waziri Ummy Mwalimu amewaomba wananchi kuchukua tahadhari kwani ugonjwa huu unambukizana kupitia kugusana kwa njia ya (majimaji kama vile mate, mkojo,damu au kinyesi).

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya