ZINAZOVUMA:

Uganda: Maporomoko ya taka za dampo yaua 23

Share na:

Idadi ya watu waliofariki nchini Uganda kutokana na mkasa uliotokea katika eneo la kutupa taka la Kiteezi imefikia 23, wakati Rais Yoweri Museveni akiagiza uchuguzi kufanyika kutokana na mkasa huo.

Ni mkasa uliotokana na taka kuangakia eneo la maakazi ya raia, shughuli za uokozi bado zinaendelea kutafuta manusura katika eneo la mkasa.

Ripoti zaidi zinasema miundo mbinu ya kuzuia takataka hiyo, katika eneo hilo ilivunjika Jumamosi asubuhi na kusababisha maporomoko katika eneo hilo.

Hii inakuja baada ya Meya wa Kampala Erias Lukwago mwezi Januari kuonya kuwa watu waliokuwa wanaishi katika eneo hilo walikuwa hatarini kuathiriwa kiafya na hata kuporomoka kwa takataka hizo zilizojaa kupita kiasi.

“Tulifanikiwa kuwaokoa watu kumi wakiwa hai ambapo kwa sasa wanaendelea kupata matibabu na tunatarajia kuwa watu kadhaa bado wamefunikwa.’’ Alisema Patrick Onyango ni msemaji wa polisi jijini Kampla.


Tayari rais Yoweri Museveni ameagiza kitengo maalum cha jeshi kusaidia katika juhudi za kuwatafuta watu waliotoweka na kutaka kuelezwa ni kwa nini watu waliruhusiwa kuishi katika maeneo kama hayo yenye hatari.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya