Wakuu wa Ulinzi wa Jumuiya ya ECOWAS wanakutana nchini Ghana leo Alhamisi na Ijumaa kukamilisha maandalizi ya kutumwa kwa Kikosi cha Kudumu cha kurejesha demokrasia nchini Niger.
Haya yanajiri kufuatia uamuzi wa wakuu wa nchi wa ECOWAS kukituma kikosi hicho baada ya juhudi za kidiplomasia kushindwa kuleta matokeo chanya ya kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa Mohamed Bazoum.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS inazidisha maradufu tishio lake la kuingilia kijeshi kurejesha utawala wa kikatiba nchini Niger baada ya serikali ya kijeshi kuchukua mamlaka mwezi uliopita.
Wakuu hao wa ulinzi wanakutana katika makao makuu ya jeshi la Ghana nchini Burma ili kupanga mkakati madhubuti wa hatua ya kijeshi nchini Niger.
Majadiliano hauo yatazingatia, rasilimali, idadi ya wanajeshi wanaohitajika, na utaratibu wa kawaida wa kufanya kazi kwa wanajeshi wa kivita.