Mahakama Kuu Mbeya leo Jumatatu, Agosti 7, imesogeza mbele uamuzi wa kesi ya mkataba wa kupinga mkataba wa bandari hadi Alhamisi Agosti 10, 2023.
Uamuzi huo wa kesi ya kupinga mkataba wa ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii, kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai (IGA), unaohusu uwekezaji katika Bandari za baharini na katika maziwa nchini Tanzania ulitakiwa ufanyike leo 7 Agosti, 2023.
Kesi hiyo imehairishwa kwasababu mwenyekiti wa jopo hayupo amepata dharura.
Uamuzi huo ulipangwa kutolewa na jopo la majaji watatu walioisikiliza kesi hiyo linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji Mustafa Ismail na Abdi Kagomba.