ZINAZOVUMA:

Tshisekedi aunda njama kumpindua Kagame

Jarida la News times la nchini Rwanda linamshutumu Raisi wa...

Share na:

Gazeti la linalounga mkono serikali ya Rwanda la The New Times limedai kuwa Rais wa Kongo Felix Tshisekedi alikutana na wapinzani wa Rwanda walio uhamishoni mjini New York tarehe 20 Septemba kujadili mipango ya kumpindua Rais Paul Kagame.

Jarida hilo lilisema mkutano huo unafuatia mkutano mwingine uliofanyika hapo awali katika ikulu ya Kinshasa tarehe 22 Mei 2023 ambao ulijadili kuunganisha makundi hasi ya Rwanda ili kuipindua serikali mjini Kigali, ikinukuu chanzo kisichojulikana.

Gazeti la New Times lilisema mkutano huo ulihudhuriwa na
Eugene Richard Gasana, aliyekuwa mwakilishi wa kudumu wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa ambaye alitofautiana na Kagame kuhusu mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo mwaka 2015.

Ukitoa gazeti hilo hakuna taarifa rasmi za kuthibika juu ya mpango huo dhidi ya Rais Kagame.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya