ZINAZOVUMA:

Tanzania na Kenya kushirikiana katika usafirishaji.

Shirika la ndege nchini Tanzania ATCL na shirika la ndege...

Share na:

Shirika la ndege la Tanzania ATCL na shirika la ndege la Kenya KQ yapo kwenye mazungumzo kuhusu ushirikiano katika usafirishaji wa mizigo.

Mashirika haya makubwa mawili yanalengo la kujiboresha na kuongeza thamani huku wakipunguza gharama za uendeshaji kwa kutumia ndege, vifaa na wataalamu waliopo.

Uhusiano kati ya ATCL na KQ unatarajiwa kutengeneza fursa za kibiashara na kufikia malengo ya soko ya kusafirisha mizigo duniani kote na bidhaa mbalimbali.

Tayari wawakilishi kutoka Tanzania kwa niaba ya ATCL na wawakilishi kutoka Kenya kwa niaba ya KQ wamekutana na mazungumzo yanaendelea kuhusu maendeleo ya ushirikiano huo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya