ZINAZOVUMA:

Tanzania kuwarejesha wanafunzi walioko Sudan.

Nchi mbalimbali Afrika na nje ya Afrika zimeanza utaratibu wa...

Share na:

Ikiwa imefikia siku 11 tangu mapigano nchini Sudan yaanze kati ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya wanamgambo wa Rapid Support Force RSF raia wa Sudan na raia wa nchi jirani ndio wanaoathirika zaidi na mzozo huo.

Hatua hiyo imepeleka nchi mbalimbali kuanza utaratibu wa kuwaondosha raia wao kutoka Sudan na kuwarejesha nchini kwao kulinda usalama wao.

Tayari serikali ya Taanzania kupitia wizara ya mambo ya nje imewaondosha wanafunzi wote wa kitanzania nchini Sudan na kwa kua safari za ndege zimesitishwa wanafunzi hao watapitia boda za nchi hio kuelekea nchini Ethiopia kwa usafiri wa basi, na baada ya hapo kwa ushirikiano wa balozi wa Tanzania nchini humo watapanda ndege kurudi nyumbani.

Kwa upande mwingine Wizara ya mambo ya nje ya Ghana ilisema raia wake walioathiriwa na mzozo huo wako salama huku Nigeria ikipanga kuwahamisha raia 5,500 kuelekea Misri huku wengi wao wakiwa ni wanafunzi.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya