Serikali ya Uganda imetoa agizo kwa watoa huduma za mtandao kuzuia tovuti za ngono ili kuwalinda vijana wa taifa hilo kutokana na athari zinazotokana na maudhui hayo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Naibu Spika wa Bunge la Uganda, Thomas Tayebwa kuagiza Serikali kuzuia maudhui yote ya ngono ili kuwalinda vijana wasio na hatia dhidi ya walaghai wa mitandaoni na machapisho ya mitandao ya kijamii yasiyofaa.
Mnamo mwaka wa 2017, Serikali ya Uganda iliunda kamati ya kudhibiti maudhui ya ngono iliyopewa jukumu la kugundua na kupiga marufuku picha hizo ndani ya mipaka ya nchi.
Kamati hii iliweza kufikia hata kutumia TZS milioni 208 kupata mashine maalum ambayo inaweza kugundua maudhui yote ya picha za ngono nchini Uganda.