Raisi wa Hungary, Katalin Novak anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo Julai 17, 2023 kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Kiongozi huyo anawasili nchini kwa mwaliko wa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na atakuwa nchini kwa siku nne kuanzia leo hadi Julai 20 mwaka huu.
Katalin ni mwanasiasa maarufu nchini Hungary ambaye alichaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo katika uchaguzi wa mwaka jana.
Kiongozi huyo ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa urais nchini humo na pia ndiye Rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Hungary ambapo alichaguliwa akiwa na umri wa miaka 44.
Kabla ya kushika wadhifa huo wa urais mwanamama huyo alikuwa Waziri anayehusika na Sera za Familia.