Marais wa nchi mbili za Tanzania na Uganda wamezindua mradi kimakakati wa umeme Afrika Mashariki ujulikanao kama Kikagati Murongo Hydropower Plant, wenye uwezo wa kuzalisha megawati 14 ambazo zitanufaisha nchi hizo mbili.
Mradi huo unaotokana na maji ya Mto Kagera, umegharimu dola za Kimarekani milioni 56, na umezinduliwa leo Mei 25, 2023 wilayani Isingiro nchini Uganda na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishirikiana na Rais wa Uganda, Yoweli Kaguta Museveni.
Akiongea na waandishi wa habari mmoja wa viongozi waandamizi katika Wizara zinazosimamia nishati kwenye nchi hizo, amesema mradi ulianza kutekelezwa 2017 na kukamilika 2022 na tayari wananchi wa nchi hizo wananufaika na matunda yake.