ZINAZOVUMA:

Raia wa Ufaransa na Ulaya waondoka Niger

Ndege ya kwanza iliyobeba raia wa Ulaya imeondoka nchini Niger...

Share na:

Ndege ya kwanza kati ya ndege tatu za kuwaondoa raia wa Ufaransa na Ulaya nchini Niger tayari imeondoka ikiwa ni baada ya siku sita tangu mapinduzi ya kijeshi kufanyika Niger.

Kuondolewa kwa Rais wa Niger aliyekuwa akiungwa mkono na nchi za Magharibi kumeleta hofu kwa raia wa kigeni hivyo kulazimika kufanya utaratibu wa kurejea katika mataifa yao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna amesema kuwa kuna watu 262 ndani ya ndege hiyo aina ya ‘Airbus’ huku ikiwa imebeba zaidi ya watoto wachanga 10.

Colonna alisema ndege hiyo inatarajiwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Paris Roissy Charles de Gaulle nchini Ufaransa.

Mapinduzi ya kijeshi ya kumuondoa Rais wa Niger Mohamed Bazoum yaliyofanywa na walinzi wake, yalisababisha wasiwasi nchini Ufaransa ambae ni mtawala wa zamani wa kikoloni wa Niger na mshirika wake wa muda mrefu.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya