Wakati akizungumza na wahitimu wa kijeshi na vyombo vya sheria Jijini Moscow, Rais Putin alieleza utayari wake wa kushiriki majadiliano kuhusu masuala ya usalama na nchi wanachama wa NATO.
Na kusema kuwa alitoa maono yao juu ya usalama sawa katika ukanda wa Eurasia, katika mkutano na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje.
Tuko tayari kwa majadiliano mapana kimataifa kuhusu masuala muhimu ya Usalama, kwa kushirkiana na wenzetu wenye mrengo huo watakapokuwa tayari katika hili.
Miongoni mwa mashirika aliyoyataja ni Shirika la Ushirikiano wa Shanghai (SCO) lililoundwa na urusi na China, pamoja na Jumuiya ya Uchumi ya Eurasia ambayo inajumuisha mataifa yaliyowahi kuwa ya Soviet.
Pia alitaja mashirika mengine kama Umoja wa mataifa huru ya Commonwealth (CIS), BRICS, nchi za Ulaya na mashirika mengine ya kimataifa ikiwemo NATOkama watakuwa tayari kwa majadiliano.
Mbali na Putin kukaribisha majadiliano ya kiusalama kwa jumuiya hizo za kimataifa, pia aliahidi kuboresha uwezo wa nyuklia wa taifa lake na kuongeza silaha za kisasa.
“Tutawajali wanajeshi walioko mstari wa mbele kwa kuwapelekea ndege zisizo na rubani, magari ya kivita, silaha za ubora wa hali ya juu, ndege za mashambulizi, mifumo ya kugundua adui, mifumo ya kutambua makombora pamoja na mifumo ya udhibiti na mawasiliano,” alisema Putin.
Na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Andrei Belousov alizungumza baada ya Putin na kuwasifu wanajeshi wa Urusi kwa heshima na utii pamoja na kujitoa katika kupambana na wafuasi wa itikazi za wanazi.