Baada ya Rais Vladimir Putin wa Urusi kuapishwa, ametangaza kubadili safu yake ya maafisa wa ulizi na usalama nchini humo.
Na katika hatua za mwanzo za kutekeleza asma yake hiyo, amembadilisha amemuondoa Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu katika nafasi hiyo, na badala Andrei Belousov atashikilia nafasi ya Waziri wa Ulinzi.
Andrei Belousov ni mchumi aliyebobea ila hana historia wala uzoefu na masuala na kijeshi.
Na badala yake Shoigu atakuwa katibu wa Baraza la Usalama la Urusi, ambalo hushauri juu ya masuala na mikakati ya kijeshi.
Wakati huo huo taarifa hiyo haijasema aliyekuwa katibu wa baraza hilo Nikolai Patrushev, ambaye pia ni mtu wa karibu na Putin atapangiwa kazi gani.
Pia katika mabadiliko hayo ya uongozi Dimitry Patrushev, mtoto wa Nikolai Patrushev ameteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu anayeshughulikia Kilimo na Ekolojia, kabla ya hapo alikuwa Waziri wa Kilimo.
Msemaji wa Ikulu ya Urusi amesema kuwa hana la kusema juu ya hatma ya Patrushev, ila taarifa rasmi zitatoka leo siku ya jumatatu.
Hadi sasa washirika wengi wa Putin bado wameshikilia nyadhifa zao kama Segei lavrov waziri wa mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi Valery Gerasimov.
“Hatua ya kumuweka Belousov kama waziri wa Ulinzi badala ya Shoigu, itamuwezesha kupambana na rushwa iliyokithiri katika wizara hiyo” alisema Philip Ingram Shushushu wa zamani wa Uingereza na bwana mipango wa NATO.
Wakati Putin akipanga safu yake ya kijeshi baada ya kuapishwa, silaha, risasi, na vifaa vingine vya kijeshi kutoka Marekani na Umoja wa Ulaya, vimeanza kufikia majeshi la Ukraine katika wiki za hivi karibuni.