ZINAZOVUMA:

Polisi wagoma kutumia silaha kisa mwenzao kushtakiwa

Polisi jijini London wamegoma kutekeleza majukumu yao Kwa kutumia silaha...

Share na:

Zaidi ya askari 100 wa jeshi la polisi jijini London, Uingereza wamekataa kutumia silaha baada ya mwenzao kushitakiwa kwa kumpiga risasi kijana wa Kiafrika.

Uingereza imeamua kuyaweka majeshi yake katika tahadhari baada ya idadi hiyo kubwa ya polisi wa London kukabidhi silaha zao wakimuunga mkono afisa mwenzao.

Wizara ya ulinzi wa Uingereza imethibitisha kwamba kwa sasa itasaidia baadhi ya majukumu ya polisi na hususan ya kupambana na ugaidi.

Polisi wengi nchini humo kwa kawaida huwa hawabebi silaha na wachache ambao huruhusiwa kujihami na silaha huwa wamepatiwa mafunzo ya hali ya juu.

Kulingana na vyombo vya habari, zaidi ya polisi 100 wa London wamejitenga na majukumu yanayohitaji silaha mpaka sasa.

Polisi huyo aliyetajwa kama NX121 alishitakiwa kwa kumpiga risasi kijana wa kiafrika wa miaka 24, Chris Kaba, kesi inayorejesha madai ya ubaguzi wa rangi ndani ya jeshi hilo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya