ZINAZOVUMA:

PANDE ZILIZOHASIMIANA SUDAN KUKUTANISHWA PAMOJA

Share na:

Maofisa wa Umoja wa Mataifa (UN) wanatarajiwa kukutana mjini Geneva, Uswisi na pande zinazohasimiana nchini Sudan katika juhudi za kutafuta suluhu ya kisiasa kwa mgogoro unaoendelea nchini humo.

Kwa mujibu wa DW, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameliambia Shirika la Habari la Al Arabiya la Saudi Arabia kuhusu mkutano huo, ingawa hakufichua tarehe rasmi ya mazungumzo hayo.

Guterres amesema Umoja wa Mataifa umehakikishiwa kuwa njia za kuingia mji wa El-Fasher ambao bado umekatiwa mawasiliano, zitafunguliwa hivi karibuni huku RSF ikiendelea kudhibiti upatikanaji wa huduma za intaneti na setelaiti za Starlink.

Tangu Aprili 2023, jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo wa RSF vimekuwa vikipigana na kusababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwafanya takriban watu milioni 12 kuhama makazi yao.

Matumaini ya kupatikana kwa mwanga katika mazungumzo kuhusu vita vya Sudan yaliongezeka mwezi uliopita baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kueleza utayari wa kusaidia kuumaliza mgogoro huo kufuatia ombi la mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman wakati wa ziara yake mjini Washington, Marekani.

Endelea Kusoma