Mratibu wa elimu ya afya kwa umma mkoani Mwanza, Leonard Mlyakado ameonya watu kula nyama pori kwani baadhi ya wanyama pori ni chimbuko la virusi vya Marburg.
Mratibu ameeleza endapo mtu yoyote atamshika au kula nyama ya mnyama mwenye virusi hivyo basi ataambukizwa virusi vya Marburg.
Ameyazungumza hayo katika mkutano wa kutoa elimu ya kujikinga dhidi ya Marburg uliohudhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini na wafanyabiashara.
Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia kuibuka kwa ugonjwa mpya wa Marburg, ambao uliripotiwa mkoani Kagera hivi karibuni.