ZINAZOVUMA:

Mwanasiasa ashtakiwa kwa kujihusisha na uchawi

Mwanasiasa wa upinzani nchini shelisheli anashtakiwa kwa kujihusisha na masuala...

Share na:

Mahakama nchini Ushelisheli imemshtaki kiongozi wa chama kikuu cha upinzani na watu wengine saba kwa tuhuma za uchawi.

Patrick Herminie ambae anapanga kugombea katika uchaguzi wa urais wa 2025 chini ya bendera ya United Seychelles Party (USP) ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini humo.

Hata hivyo, amekanusha mashtaka hayo na kusema kuwa kukamatwa kwake na kufunguliwa mashtaka ni juhudi za kisiasa za kuchafua taswira yake na ya chama chake.

Polisi wanasema kisa hicho kinahusiana na kupatikana kwa miili miwili iliyokuwa imetolewa kwenye makaburi katika kisiwa cha Mahe.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo, Bw Herminie na washtakiwa wenzake wanakabiliwa na mashtaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na kupatikana na vitu vilivyoshukiwa kutumiwa katika uchawi na kula njama ya kufanya uchawi.

Polisi wanasema walimpata Bw Herminie akiwa na stakabadhi zinazoshukiwa kuibwa kutoka maeneo yaliyoharibiwa yakiwemo makanisa ya Kikatoliki.

Pia wanadai kuwa jina la Bw Herminie lilionekana kwenye mawasiliano ya Whatsapp kati ya raia wa Ushelisheli na Mtanzania ambaye alikamatwa Septemba akiwa na vitu vinavyohusiana na uchawi.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya