Mwanajeshi mmoja kutoka nchini Congo katika jimbo la Ituri anatafutwa baada ya kuwapiga risasi watu 13, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Luteni Jules Ngongo, msemaji wa utawala wa kijeshi katika mkoa wa Ituri alisema akizungumza na vyombo vya habari kuwa popote pale askari huyo atakapokwenda watamkamata.
Kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo kati ya watu 13 waliofariki, tisa ni watoto, huku taasisi inayofuatilia masuala ya kiusalama katika jimbo la Kivu Baromètre Sécuritaire du Kivu ikisema kuwa wawili ni wanawake.
Askari huyo wa jeshi la serikali anatuhumiwa kuwaua watu hao Jumamosi usiku katika eneo la Tchomia karibu na Ziwa Albert jimbo la Ituri.