ZINAZOVUMA:

Museven aijibu Benki ya Dunia

Raisi wa Uganda Yoweri Museven amesema nchi yake itaendelea kwa...

Share na:

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameishutumu Benki ya Dunia kwa kutumia pesa kujaribu kuishinikiza serikali yake juu ya sheria yenye utata dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Kauli ya Rais Museveni imekuja baada ya tangazo la Benki ya Dunia kwamba inasitisha mikopo mipya kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki kutokana na kupitisha sheria kali zaidi dhidi ya LGBTQ.

Benki ya Dunia ilisema kuwa Sheria ya Uganda ya Kupinga Ushoga inakinzana na maadili ya taasisi hiyo na kwamba hakuna ufadhili mpya wa umma utakaowasilishwa kwa bodi yake ya wakurugenzi ili kuidhinishwa kwa sasa.

Lakini Museveni, ambaye alitia saini hatua hizo kuwa sheria mwezi Mei, aliandika katika mtandao wake wa Twitter kwamba “Waganda wataendelea iwe kwa mikopo au bila mikopo”

“Inasikitisha kwamba Benki ya Dunia na wahusika wake wanathubutu kutaka kutulazimisha kuacha imani, utamaduni, kanuni na uhuru wetu kwa kutumia pesa,” Rais Museven alisema.

“Hatuhitaji shinikizo kutoka kwa mtu yeyote kujua jinsi ya kutatua matatizo katika jamii yetu.”

Hata hivyo Museven alisema Uganda itaendelea na majadiliano na Benki ya Dunia ili waweze kuepuka upotoshaji huu kama ikiwezekana.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya