ZINAZOVUMA:

Muhimbili kuamua hatma ya Mandonga

Bondia Karim Mandonga anasubiri majibu ya vipimo alivyofanya katika hospitali...

Share na:

Bodia Karim Mandonga amefika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanya vipimo kuangalia afya yake baada ya kuhitajika kufanya hivyo kabla ya pambano lake la tarehe 27 mwezi huu.

Mandonga amesema ni utaratibu wa kawaida kujua afya kabla ya kupanda ulingoni na anasubiri majibu kutoka kwa wataalamu wa afya.

Aidha amebainisha kuwa amepata huduma Bora kutoka kwa mdaktari na vifaa vya kisasa vilivyotumika kumfanyia vipimo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hatua ya Mandonga imekuja baada ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) kumtaka apime afya yake baada ya kupigwa TKO katika pambano lake na Moses Golola kutoka Uganda lililofanyika Julai 29, 2023 jijini Mwanza.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya