Kampuni maarufu kwa kutengeneza poda za watoto duniani ya Johnson & Johnson imekiri kutakiwa kulipa Dola Bilioni 8.9 za Kimarekani ambazo ni sawa na shilingi Trilioni 20.8 za Tanzania.
Pesa hizo zitalipwa ndani ya kipindi cha miaka 25, kama suluhisho kwa madai ya bidhaa yake ya poda kusababisha Saratani kwa watumiaji.
Kampuni hiyo imekwishasitisha uuzaji wa poda za watoto zenye ‘Talc’ duniani kote mwaka huu, baada ya kukabiliwa na maelfu ya kesi kutoka kwa wateja wakidai bidhaa za poda zenye ‘Talc’ zimesababisha Saratani kutokana na kuweka mazingira rafiki kwa visababishi vya ugonjwa huo.