Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nauye amesema katika kuhakikisha wanapambana na mapenzi ya jinsia moja na wale wanaotangaza mambo hayo serikali imefungia tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198, Twitter 12 vikoa zaidi ya 2,456.
Aidha kwa upande mwingine akijibu swali aliloulizwa Bungeni Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Philipo Gekul amesema “Kifungu cha 9 cha Sheria ya Ndoa kinatafsiri Ndoa ni mahusiano ya hiyari kati ya Mwanaume na Mwanamke.
Ameongeza “Pia Kifungu cha 154 cha Sheria ya Kanuni za adhabu Sura ya 16 kinabainisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kufungo cha maisha jela au kisichopungua miaka 30 jela.”