Ripoti ya C.A.G 2021/2022 imebaini kuongezeka kwa gharama za ununuzi wa Treni ya kisasa (SGR) kwa Tsh. Bilioni 492.46 na Mabehewa ya Abiria kwa Tsh. Bilioni 11.59 kutokana na usimamizi duni wa Mikataba
Pia, Mkataba ulitekelezwa bila kuwepo kwa dhamana ya utendaji na kusababisha hasara ya Tsh. Bilioni 13.6 kutokana na kutotoza gharama za ucheleweshaji wa kazi kwa mujibu wa Mkataba.
Kwa upande mwingine pia ripoti hiyo imebaini vituo binafsi vya Huduma za afya vilikuwa na kiwango kikubwa cha madai yasiyostahili katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Udanganyifu huo ulisababisha zaidi ya Tsh. Bilioni 10.4 kulipwa kwenye Vituo binafsi kuanzia Mwaka 2019/20 hadi 2021/22, Vituo vya Serikali Tsh. Bilioni 1.6 na vituo vya Taasisi za Kidini Tsh. Bilioni 2.5.
Kwa upande mwingine pia vyama mbalimbali vya upinzani nchini vimefanya uchambuzi wa ripoti hiyo na kutoa mapendekezo kwa serikali ikiwemo chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA pamoja na chama cha ACT Wazalendo.