ZINAZOVUMA:

MAREKANI umewaonya raia wake waliopo Nairobi kupitia ubalozi

Ubalozi wa Marekani wa Nairobi watoa tahadhari kwa raia wake...

Share na:

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa tahadhari ya usalama kwa raia wake wanaoishi jijini Nairobi kutokana na ongezeko la vitendo vya uhalifu katika maeneo ya makazi ya watu.

Kulingana na tahadhari iliyotumwa kwenye tovuti ya ubalozi siku ya Ijumaa, uhalifu huo ni pamoja na uporaji wa mikoba na simu.

Katika taarifa hiyo ya ubalozi imewataka raia wa marekani kuchukua tahadhari ikiwemo zifuatazo

Mosi, Kujihadhari katika mazingira waliyopo, Pili Kuchukua tahadhari katika nyendo zao, tatu Kutoonesha dalili za utajiri, kama vile kuvaa vito vya thamani au saa, au kutembea na pesa nyingi.

Nne wasikabiliane dhidi ya jaribio lolote la kimwili dhidi ya jaribio lolote la wizi na wabaki watulivuili kuepusha kusababisha vurugu. Na mwisho kufunga milango ya magari na madirisha katika msururu.

Balozi za marekani na nchi za magharibi zimekuwa zikitoa taarifa za namna hii kwa raia wake mara kwa mara, na hata kuzichapisha katika tovuti za balozi zao kwa ajili ya kuwaepusha na mazingira hatarishi.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya